Pata taarifa kuu
JAPAN-MASUZOE

Mkuu wa mkoa wa Tokyo ajiuzulu

Mkuu wa mkoa wa Tokyo, Yoichi Masuzoe, anayetumiwa kutumia fedha za kisiasa kwamaslahi yake binafsi, alijiuzulu leo Jumatano masaa machache tu kabla ya Wabunge kupiga kura ya kutokua na imani naye, kituo cha habari cha serikali cha NHK kimearifu.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe (kushoto) na mkewe Akie Abe Juni 16, 2013.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe (kushoto) na mkewe Akie Abe Juni 16, 2013. REUTERS/Peter Andrews
Matangazo ya kibiashara

Kujiuzulu kwa mwanasiasa huyo, mwenye umri wa miaka 67, aliyeshiriki sana katika maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2020, ni pigo kubwa kwa kamati ya maandalizi ya tukio hilo, ambalo tayari limekubwa na kashfa kadhaa.

Yoichi Masuzoe amemueleza Spika wa Bunge katika mji mkuu uamuzi wake, kituo cha habari cha serikali cha NHK na vyombo vingine vya habari vimearifu. Manispaa ya Tokyo, haikuweza kuthibitisha taarifa hii mara moja.

Vyama tisa vya kisiasa, vikiwemo vile viliounga mkono kugombea kwake 2014, vimekua vikidai kujiuzulu kwa Bw Masuzoe, ambaye atajiuzulu rasmi Juni 21.

Yoichi Masuzoe alishindwa kuonyesha jinsi pesa alizokua akisimamia zilivyotumika. Ubadhirifu huo uligunduliwa na vyombo vya habari mwishoni mwa mwezi Aprili.

Alikiri kuwa alitangaza kimakosa kama gharama alizofanya kama kiongozi aliyechaguliwa alizifanya kwa pesa zake binafsi, hususan manunuzi binafsi, ikiwa ni pamoja na kukaa na familia yake katika hoteli ya kifahari au kutumia gharama ghali katika migahawa mbalimbali ya kifahari. Kamati ya wataalam wa kisheria iliyoteuliwa kwa kusimamia huduma zake imetaja kwa alitumia fedha nyingi, lakini imesema kuwa utaratibu aliyotumia ni kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.